Home Campus Directory | A-Z Index

 

Watuma maombi wa kimataifa ni wale wote wanaohitaji visa kuweza kuchukua masomo katika Chuo Kikuu cha Penn State.

Chuo Kikuu cha Penn State ni miongoni mwa vyuo 10 vikubwa kuliko vyote Marekani.  Dhima yake ni kuboresha maisha ya watu katika jimbo la Pennsylvania, nchini, na kote duniani kwa kutumia programu zake unganishi za ufundishaji, utafiti, na utoaji huduma kwa umma.  Yafuatayo ni maelezo kwa kifupi.

Tawi la Brandywine la Chuo Kikuu cha Penn State ni la kutwa (halina mabweni).  Lina wanafunzi wazawa wa nchi 60.

Kwa kuwa tuko karibu na jiji la Philadelphia, tawi letu lina mazingira ya kukaribisha na lina mchanganyiko wa watu.

Japo matawi yote ya Chuo Kikuu cha Penn State hupokea wanafunzi wa kimataifa, tofuti (website) yetu Undergraduate Admissions ina maelezo kamili kwa wanafunzi wa kimataifa wanaotaka kutuma maombi kwa tawi letu.